Mtoto Hamis Hashim Bakari.

Hamis akiwa na mmoja wa ndugu zake.

...akiwa na mwanahabari wetu, Chande Abdallah.
Chande Abdallah na Denis Mtima Tafadhalini msaada wadau! Mtoto Hamis Hashim Bakari, mwenye umri wa miaka 13, anapata mateso makubwa akisumbuliwa na tatizo la miguu kujaa maji kutokana na kugundulika kuwa na mifupa laini tangu mwaka 2008.
Mtoto Hamis anaishi na wazazi wake Yombo Dovya, jijini Dar. Tatizo lake lilianza alipovunjika mguu wa kushoto ambao ulijaa maji na kuvimba.
Katika harakati za kupata matibabu, Hamis alitibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kugundulika tatizo na akawa ameshindwa kutembea huu mwaka wa tano sasa.
Muda wote Hamis anatambaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine huku safari ndefu akizifanya kwa msaada wa baiskeli aliyopewa na Shule ya Msingi ya Yombo Dovya.
Kufuatia mateso anayopata kila kukicha, Mtoto Hamis anaomba wasamaria wema kutoka sehemu mbalimbali wamsaidie ili kufanikisha matibabu na huduma nyingine.
Mwenye msaada wowote wa hali na mali kwa Mtoto Hamis, tuma au wasiliana na simu namba 0784211085 au 0714452275.