MSHTUKO mkubwa ulijiri Jumamosi iliyopita, ikiwa ni baada ya kusambaa kwa habari za kumwagiwa tindikali, mfanyabiashara mwenye ‘levo’ ya ubilionea, Said Said Mohammed, 42, ambaye ndiye mmiliki na Mkurugenzi Mkuu wa Home Shopping Centre.
Nje ya jengo la Msasani Mall ambapo Said Said Mohammed alimwagiwa tindikali. Katika jengo hili kuna maduka ya mfanyabiashara huyo.
Said ambaye kwa utambulisho mwingine anajulikana kama Said Mohammed Saad, alimwagiwa tindikali Ijumaa iliyopita, saa 2 usiku, lakini habari zake zikavuma Jumamosi, hivyo kuibua taharuki ya aina yake.
Duka lingine analomiliki mfanyabiashara huyo.
Kuhusu nani alimmwagia tindikali hiyo, sababu ya kutendwa unyama huo, yupi mhusika mkuu wa ukatili wenyewe na malengo ya uharamia, kwa jumla, hayo ni maswali yanayoendelea kuitesa familia yake, watu wa karibu pamoja na Jeshi la Polisi Tanzania.
Taarifa za kipolisi zinathibitisha kwamba alimwagiwa tindikali akiwa anazungumza na mfanyakazi wake wa duka lake lililopo kwenye Jengo la Msasani City Mall kisha akakimbizwa Hospitali ya Ami Wellness Centre, iliyopo Masaki, Dar es Salaam kabla ya kupelekwa Afrika Kusini kwa ndege ya kukodi ndani ya kipindi kisichozidi dakika 60.
SAID NI NANI?
Ni Mtanzania mwenye asili ya Bara la Asia. Inadaiwa kwamba ndugu zake wengi wana asili ya nchi za Yemen na Saudi Arabia.
Ndiye mmiliki wa Kampuni ya Home Shopping Center. Kampuni hiyo ina maduka mengi Dar es Salaam na katika mikoa kadhaa ambayo yanahusika zaidi na uuzaji wa vitu vya nyumbani na ofisini.
Anatajwa kuwa tajiri mwenye uwezo zaidi katika jumuiya ya wafanyabiashara wa eneo la Kariakoo, kifedha na ushawishi.
Inadaiwa kwamba wafanyabiashara wengi wenye maduka yao Kariakoo, humtegemea yeye kuingiza mizigo nchini, kutokea nje ya nchi hususan China.
Anamiliki nyumba kadhaa za ghorofa Kariakoo, yapo madai kwamba anamiliki nyumba sita.
Baadhi ya majengo ambayo anahusishwa nayo, la kwanza lina ghorofa saba, lipo Mitaa ya Swahili na Msimbazi, la pili lina ghorofa sita, lipo Kongo na Aggrey, tatu ni la ghorofa nne, lipo Barabara ya Uhuru na kadhalika.

0 Comments