Zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Zimbabwe, maafisa wa usalama nchini humo wamepiga kura ya mapema.
Zoezi hilo limekumbwa na ucheleweshaji uliosababishwa na ukosefu wa karatasi za kupigia kura.
Maafisa wa polisi waliovalia sare wamepanga msitari nje ya vituo vya kupigia kura jana Jumapili, huku tume ya uchaguzi ikiendelea kuchapisha makaratasi ya kura.
Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha MDC Bw. Morgan Tsvangirai ambaye pia ni Waziri Mkuu katika serikali ya umoja wa kitaifa, amesema hitilafu za jana zilidhihirisha mashaka juu ya uwezo wa tume ya taifa ya uchaguzi kuendesha uchaguzi huo kwa ufanisi.-DW.