Raia wa Zimbabwe wanapiga kura katika uchaguzi wa Urais unaotajwa kuwa na
ushindani mkali huku kukiwa na madai ya udanganyifu. Rais Robert Mugabe wa miaka
89 amesema atang'atuka ikiwa yeye na chama chake cha Zanu-PF watashindwa.
Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai na chama chake cha Movement for Democratic Change
(MDC) wamelalamikia Zanu-PF kwa kuhitilafiana na utaratibu wa uchaguzi ili
kunyakua ushindi, lakini chama tawala kimekanusha madai hayo.Shughuli za
kampeini zimekua ghasia zozote huku kukiwa na visa vichache sana vya kuwatisha
wapiga kura.
Vyama vya Zanu-PF na MDC viliunda serikali ya muungano mwaka wa 2008 baada ya
muafaka wa kumaliza ghasia za baada ya uchaguzi kufuatia matokeo ya Urais
yaliyozua utata. Bw.Tsvangirai alishinda awamu ya kwanza, lakini akajiondoa kwa
raundi ya pili akilalamikia mashambulizi yaliyolenga wafuasi wake.
Serikali ya Zimbabwe imewapiga marufuku waangalizi wa magharibi kuchunguza
uchaguzi wa leo. Hata hivyo Muungano wa Afrika{AU}, Kanda ya Kusini mwa
Afrika{SADC} na makundi ya kijamii nchini Zimbabwe yamekubaliwa kufuatilia jinsi
uchaguzi utakavyoendeshwa.
Watu milioni 6.4 wamejiandikisha kupiga kura hii, na maelfu walijitokeza
kwenye kampeini za uchaguzi. Matokeo yanatarajiwa kutolewa kwa siku tano
zijazo.Mwandishi wa BBC aliyeko Harare amesema kuna foleni ndefu katika vituo
vya kupigia kura leo ikiwa siku ya mapumzoko kuhakikisha raia wanapata nafasi ya
kuamua serikali mpya.
Mshindi wa moja kwa moja sharti apate asili mia 50 ya kura zote kutangazwa
Rais. Ikiwa hakuna mgombea atapata kura hizo, raundi ya pili imepangwa kufanyika
Septemba 11. Uchaguzi huu ndio wa kwanza kufanyika Zimbabwe chini ya katiba mpya
iliyopitishwa mnamo mwezi
0 Comments