Hili ni soko la Darajani Zanzibar, ni baadhi tu ya maeneo ambayo bidhaa za wakulima wa horticulture Zanzibar upelekwa na kuuzwa kwa ajili ya kukizi haja za soko la ndani.
Mkurugenzi wa TAHA akiteta Jambo na Mtaalamu wake kwa upande wa Visiwani Mzee Biwi wakati alipotembelea moja ya mashamba ya tikiti maji ya wakulima ambao ni wanachama wa TAHA.

Wataalamu kutoka Finland ambao ndio wawezeshaji wa shughuli za TAHA Zanzibar wakitazama moja ya shamba la Matikiti maji la moja ya vikundi wanachama wa TAHA.

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo na Maliasili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mtumwa Kheir Mbarak akihutubia wakati wa sherehe fupi za ufunguzi wa ofisi hizo za Tanzania Horticultural Association (TAHA) 

Mkurugenzi wa TAHA, Bi Jacqueline Mkindi akisema neno la ufunguzi kwa Mh. Mtumwa Kheir Mbarak na wageni waharikwa wakati wa sherehe hizo za ufunguzi wa Ofisi za TAHA-Zanzibar

Moja ya mashamba darasa ya TAHA yaliyopo eneo la Donge, Wilaya ya Kaskazini Unguja

Wakulima wanaojishughulisha na kilimo cha Mazao ya horticulture wakiwa katika moja ya Warsha zilizoandaliwa na TAHA masaa machache kabla ya ufunguzi wa ofisi hizo kisiwani hapo.

PICHA NA MAELEZO KWA IHSANI YA MICHUZI