Ibara ya 31 katika eneo la uhuru wa imani ya dini inasema kila mtu anao uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya ya imani ya dini, imani yake au kutokuwa na imani na dini.

Sumbawanga.
BAADHI ya wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, wametaka katika katiba ijayo kuwe na muundo wa Serikali moja, huku Zanzibar ikiwa ni moja ya mikoa ya nchi ya Tanzania na iwapo Wazanzibari watakataa, waruhusiwe kujitenga.
Mmoja wa wajumbe wa baraza hilo la Katiba Wilaya ya Kalambo, Afred Ntinda mkazi wa kata ya Mwazye kijiji cha Mpenje alisema hayo jana wakati akichangia maoni katika kikao cha baraza hilo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya mjini hapa.
Mpenje alisema kuwa mfumo wa sasa wa Serikali mbili una kasoro nyingi na umeshindwa kutatua kero za Muungano hivyo hautakiwi kuendelea kuwepo wakati ule wa Serikali tatu hawezi kulinda muungano huo kwa kuwa Serikali hizo zinaweza kuongozwa na marais kutoka vyama tofauti vya siasa na wenye mitizamo isiyolingana hivyo kuna hatari ya muungano kuvunjika.
“Sisi huku bara kuwa na Serikali moja si tatizo wengi wataridhia, nafikiri kuna tatizo katika upokeaji wa maoni kwa wenzetu wa Zanzibar.

-------------------------------------------
Na Mussa Mwangoka,Sumbawanga.