Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mlezi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania, (SHIMUTA) Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Nyaraka za Katiba ya Shirikisho hilo, kutoka kwa Mwenyekiti wake, Khamis Mkanachi, wakati Uongozi huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salam, jana Agosti 13, 2013 kwa ajili ya mazungumzo. Katikati ni Naibu Katibu wa Makamu wa Rais Mohamed Khamis.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mlezi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania, (SHIMUTA) Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Viongozi wa Shirikisho, wakati Uongozi huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salam, jana Agosti 13, 2013 kwa ajili ya mazungumzo na kumkabidhi Katiba ya Shirikisho hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mlezi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania, (SHIMUTA) Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Shirikisho hilo baada ya maongezi yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu Jijini Dar es Salaam jana. Picha na OMR