Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai yenye rangi ya taifa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi ya Dinka ya Uholanzi baada ya kuchangisha milioni themanini za ujenzi wa shule ya Dinka inayojengwa Arusha.

Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi ya DART ya Uholanzi baada ya kuzindua taasisi hiyo inayotafuta misaada ya kusaidia vijana Tanzania. Taasisi hiyo inasimamia na kuendesha kituo cha kusaidia vijana, Mwanza. Balozi Kamala amewashukuru Viongozi hao na amewaomba Watanzania wanaokaa katika nchi za Benelux kuchangamkia fursa mbalimbali zinzopatikana katika nchi za Benelux kusaidia nyumbani.