MSHAMBULIAJI Daniel Sturridge amepeleka machungu kwa wapenzi wa Manchester United baada ya kuifungia timu yake ya Liverpool bao la pekee katika mchezo wa leo.
Sturridge  amefunga bao hilo dakika ya nne ya mchezo na kuwafanya Majogoo hao wa Liverpool kuibuka na pointi tatu kwenye mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Anfield.