Grace Aikaeli Mbowe (kushoto) wakati akijiunga na CCM akitokea Chadema.
DADA wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Grace Aikaeli Mbowe, aliyejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) akitokea CHADEMA, hivi karibuni anadaiwa kufariki dunia katika ajali ya gari. Grace, mumewe na mtoto wao wanadaiwa kufariki katika ajali iliyotokea leo asubuhi eneo la  Kabuku, Segera mkoani Tanga. Gari wanalodaiwa kupata nalo ajali ni Toyota GX 100 na baada ya kadi ya gari hilo kuchunguzwa ilibainika kuwa na  jina la Grace Aikaeli Mbowe ambaye ni mmiliki.