Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akiwapa nasaha wanamichezo wa wizara hiyo katika tafrija fupi ya kuwaaga wawakilishi wa wizara hiyo ambao watashiriki katika mashindano ya Shirikisho ya Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (Shimiwi) yatakayofanyika mjini Dodoma Jumamosi. Tafrija ya kuwaaga wanamichezo hao ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Maafisa wa Polisi jijini Dar es Salaam jana.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wanamichezo wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya kuwaaaga rasmi katika tafrija iliyofanyika Chuo cha Maafisa wa Polisi, jijini Dar es Salaam jana. Abdulwakil aliwataka wanamichezo hao wahakikishe wanashirikiana ipasavyo na hatimaye wanashinda michezo aina mbalimbali inayotarajiwa kuanza mjini Dodoma Jumamosi. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 Comments