Kikundi cha Kwaya cha akina mama kinachofahamamika kwa jina la Chui kutoka Nyamajashi kikitumbuiza kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kisesa, Lamadi Wilaya ya Busega.

Kikundi cha Ngoma cha Mwanalyaku Dance Group kikionyesha uwezo wake wa kucheza ngoma ya bugobogobo ikiwa sehemu ya utangulizi kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara wa CCM uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 
Mkuu wa Wilaya ya Busega Ndugu Paul Mzindakaya katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kisesa, Lamadi na kumuambia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana maji bado ni tatizo kwa wakazi wa wilaya yake. 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Lamadi wilayani Busega kwenye Mkutano wa hadhara na kuwaambia wananchi wawe makini na makanjanja wa kisiasa ambao kwa sasa wamefunga ndoa batili kutaka kuvuruga mchakato wa kupata Katiba mpya. 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Lamadi kwenye Viwanja vya Kisesa wilaya ya Busega mkoa wa Simiyu na kuwaambia wananchi kuwa muda wa walimu kuendelea kupata tabu umeisha na kuagiza mamlaka husika kutatua kero na madai ya walimu ndani ya miezi sita na kama wameshndwa wajiuzulu kupisha watu wengine.