Hit maker wa Ngoma ya Pombe Yangu kutoka Kruu la Tip Top Connection, Hamad Ally ‘Madee’ au Rais wa Manzese amekiri kutekeza zaidi ya Shilingi milioni 168 baada ya kuangusha bonge la mjengo maeneo ya Mbezi-Shamba, Dar.
Akizungumza na Weekly Star Exclusive juzikati, Madee alifunguka kuwa kiwanja chenye ukubwa wa mita 50 kwa 50 alichojengea nyumba hiyo, alikinunua mwaka 2006 kwa shilingi milioni 6.5 ambapo hadi sasa ameshatumia kiasi hicho cha fedha na bado haijakamilika.

“Kiukweli ni nyumba kubwa na ina vyumba vingi. Kuna chumba changu, vyumba vya watoto wa kike na kiume, sebule, sehemu ya kugonga msosi, jiko, chumba cha kuangalia movies (kama studio), vyoo na mabafu.
“Pia kuna maegesho ya magari kama mawili. Nataraj ia kuhamia Aprili 23, mwakani, siku ya birthday yangu,” alisema Madee.
Kuhusu alikopata fedha hiyo huku baadhi ya wasanii wakihusishwa na usafirashaji wa madawa ya kulevya, Madee alisema zilitokana na shoo nyingi ambazo amekuwa akipiga kila wiki ndani na nje ya Bongo.
0 Comments