Na Abdulaziz Video,Masasi Katika harakati za kuboresha kiwango cha Elimu wilayani Masasi Mkoani Mtwara,Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Juma Ali Simai amezindua Chumba cha masomo ya komputa katika shule ya sekondari ya Ndanda ambalo limegharimu kiasi cha shilingi milioni 49 zilizotolewa na wahisani mbalimbali ikiwemo mamlaka ya mawasiliano nchini(TCRA). Uzinduzi huo uliofanyika katika mbio hizo utawezesha wanafunzi kupata elimu ya kompyuta na tehama ili kuwajengea uwezo wanafunzi hao kutokana na upungufu mkubwa wa Vitabu kufuatia kompyuta hizo kufungwa pamoja na huduma ya Intanet. Akizungumza wakati akizindua jengo hilo la komputa Juma Simai aliwataka wanafunzi kutumia kompyuta hizo kwa ajili ya kujifunza zaidi ili kupata elimu juu ya masomo na si kwa kuangalia mambo ambayo hayatasaidia katika maisha yao ikiwemo utandawazi unaoendelea Duniani ikiwa pamoja na mambo ambayo hayafuati maadili ya Elimu. Awali akipokea Mwenge wa Uhuru toka wilaya ya Newala,Mkuu wa wilaya ya Masasi,Bi Farida Mgomi alibainisha kuwa pamoja na wilaya hiyo kukimbiza Mwenge huo kwa kilometa 120. Miradi itakayotembelewa na kuzinduliwa kabla ya kuukabidhi katika wilaya ya Nanyumbu. Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi walioongea na globu hii walieleza kuwa uzinduzi wa Chumba cha komputa utasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha elimu yao. Mwenge ukiwa wilayani Masasi umetembelea, jumla ya miradi 10 kati ya miradi hiyo imefunguliwa,kuwekewa mawe ya msingi na kutembelewa yote ikiwa na thamani ya shilingi Bilioni 2.4 ikiwemo chumba cha kompyuta kwenye shule ya sekondari ya Ndanda,mradi wa umwagiliaji maji wa Mpowora,upandaji wa miti ya mbao katika kijij Mwenge i cha Mwen nda,ujenzi wa mahabara ya kisasa kwenye kituo cha afya cha Chiwale na kutembelea vikundi vya wajasilia mali, Pamoja na shamra hizo za mwenge pia kulipambwa na burdani ya Bendi ya Vijana Jazz ya Dar es sallam |
0 Comments