Bondia wa Tanzania, Francis Cheka (kushoto) akimtandika konde mpinzani wake Phil Williams wa Marekani katika pambano la kuwania mkanda wa ubingwa wa Dunia WBF, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Cheka alishinda kwa pointi. Picha na Michael Matemanga
Dar es Salaam.
Jina la Francis ‘SMG’ Cheka liling’ara juzi usiku kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya kutwaa ubingwa wa dunia unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi la Dunia uzani wa supermiddle.
Katika mpambano huo ulioanza saa 5:43 usiku Cheka alitwaa ubingwa huo kwa pointi dhidi ya Phil Williams wa Marekani.
Awali saa 5:32 wakati Cheka aliyeambatana na baadhi ya mashabiki wake akiwamo kocha wake, Abdallah Saleh alipanda ulingoni akitokea lango kuu la kuingia ukumbini hapo na kisha kusalimia mashabiki wake na kwenda moja kwa moja kusimama kwenye kona nyekundu.
Dakika tatu baadaye Williams alipanda ulingoni na kwenda kusimama kona ya bluu kabla ya nyimbo za mataifa yote mawili kuimbwa. Cha kufurahisha, Watanzania waliimba wimbo wa Taifa wakati wimbo wa Marekani uliimbwa na mwakilishi kutoka Ubalozi wa Marekani, Tanzania.
Baada ya yote, mwamuzi, Darryl Ribbink alianzisha pambano hilo.
Zifuatazo ni raundi 12 muhimu zilizompa ushindi Cheka kwa pointi za majaji 3-0 za 116-113, 119-108 na 117-111.
Mabondia wote wanaanza pambano kwa kuviaziana. Kila mmoja akisoma mbinu za mwenzake. Walikuwa wakitishiana na hakuna hata ngumi moja iliyorushwa zaidi ya kurukaruka.
Cheka alianza kwa ngumi za kudokoa lakini Williams anakuwa mjanja kukwepa.
Alikuwa anavizia kumpiga na mkono wa kulia lakini Cheka anakuwa makini.Wanarudia kuviziana huku kila mmoja akimtegea mwenzake. Cheka anajaribu kushambulia, anamtandika ngumi moja usoni iliyowanyanyuma mashabiki kwenye viti, lakini Williams anajibu kwa makonde mawili lakini hayakuwa na uzito.
Williams anaingia kwa kasi kujibu mashabulizi ya raundi ya pili. Cheka anakuwa makini. Anamjibu kwa ngumi mfululizo lakin Williams anajitahidi kuhimili na kukaa sawa. Cheka anashangiliwa baada ya kufanikiwa kumpa moja kali.
Cheka anakunjuka. Anamshambulia mfululizo Williams. Makonde mawili yanamlewesha Williams, anaanguka kwenye kamba za ulingo na kulamba sakafu.
Mwamuzi anamhesabia na kuamua kuendelea.
Cheka anatumia nafasi ile, anamshambulia mfululizo lakini wakati ngumi hazijamnyong’onyeza Mungu bariki, kengele inapigwa ya kumalizika dakika tatu za raundi hiyo.
Williams amepata nguvu mpya. Anaingia raundi ya tano kama kifaru aliyejeruhiwa lakini hakufika popote. Cheka anaisoma kasi yake na anamkwepa japokuwa ngumi mbili safi Cheka alikutana nazo.
Cheka anaonyesha kuyumba, lakini anaimarika na kumwanzishia mashambulizi na kutumia mbinu ya kukumbatia kabla ya mwamuzi kumuonya. Hakuna ngumi za maana zilizorushwa zaidi ya kukumbatiana.
Cheka anapata kichapo cha aina yake. Ilikuwa dakika ya pili ya raundi hii bila kujibu mashambulizi na kutumia mbinu ya kukinga kwa kukumbatia.Mwamuzi anajarimu kumuonya kuacha kukumbatia, lakini Cheka alionekana kuzidiwa ujanja.
Raundi hii kila mmoja anamshambulia mwenzake kwa zamu. Walikuwa wakitegeana kama ilivyokuwa raundi ya kwanza. Baadaye, kila mmoja alirusha ngumi za kuvizia na kudokoa kabla ya kumalizika kwa raundi.
Cheka anambadilikia mpinzani wake. Ilikuwa nafasi nzuri kwake kumaliza mpambano, lakini Williams ni mjanja pia kumsoma mpinzani wake.
Pamoja na kumsoma, Cheka anashambulia kwa kushtukiza. Anarusha makonde yanayomlevya mpinzani wake. Tatizo la Cheka anashindwa kurusha ngumi za harakaharaka hali iliyompa mpinzani wake nafasi ya kujihami na kusaidiwa tena na kengele ya kumalizika kwa muda.
Williams anamgeuzi kibao Cheka lakini hakuweza kuendelea na aina ya mchezo alioanza nao na kujikuta anapigwa yeye. Dakika ya mwisho ya raundi hii, Williams anaonekana kulewa lakini anajiimarisha.
Cheka anajikusanyia pointi baada ya kucheza ngumi za ukweli. Anambadilikia mpinzani wake na kumpiga mfululizo. Williams anajibu, lakini haonyeshi kama ana matumaini ya ushindi.
Williams alianza kucheza kwa kutegea sawa na Cheka, pengine walikuwa wakivizia raundi ya mwisho. Sekunde chache, Cheka alipata ngumi kali mbili zilizompata usoni.Mwamuzi anajarimu kumuonya kuacha kukumbatia, lakini Cheka alionekana kuzidiwa ujanja.
Raundi hii kila mmoja anamshambulia mwenzake kwa zamu. Walikuwa wakitegeana kama ilivyokuwa raundi ya kwanza. Baadaye, kila mmoja alirusha ngumi za kuvizia na kudokoa kabla ya kumalizika kwa raundi.
Cheka anambadilikia mpinzani wake. Ilikuwa nafasi nzuri kwake kumaliza mpambano, lakini Williams ni mjanja pia kumsoma mpinzani wake.
Pamoja na kumsoma, Cheka anashambulia kwa kushtukiza. Anarusha makonde yanayomlevya mpinzani wake. Tatizo la Cheka anashindwa kurusha ngumi za harakaharaka hali iliyompa mpinzani wake nafasi ya kujihami na kusaidiwa tena na kengele ya kumalizika kwa muda.
Williams anamgeuzi kibao Cheka lakini hakuweza kuendelea na aina ya mchezo alioanza nao na kujikuta anapigwa yeye. Dakika ya mwisho ya raundi hii, Williams anaonekana kulewa lakini anajiimarisha.
Cheka anajikusanyia pointi baada ya kucheza ngumi za ukweli. Anambadilikia mpinzani wake na kumpiga mfululizo. Williams anajibu, lakini haonyeshi kama ana matumaini ya ushindi.
Williams alianza kucheza kwa kutegea sawa na Cheka, pengine walikuwa wakivizia raundi ya mwisho. Sekunde chache, Cheka alipata ngumi kali mbili zilizompata usoni.RAUNDI YA 12
Cheka anacheza kwa tahadhari na kumpa nafasi mpinzani wake kushambulia lakini alimbadilikia na kujibu mashambulizi dakika ya mwisho. Williams anaonekana kuyumba, Cheka anatumia nafasi ya kushambulia lakini baadaye anapata nguvu anajibu. Cheka sasa amefikisha mikanda minane ya ubingwa ya IBC, IBO, WBC, IBU, IBO, IBF, ubingwa wa Taifa na huo aliotwaa mwishoni mwa wiki iliyopita wa WBF.
|
0 Comments