Watu waliokuwa na silaha wamefyatua risasi mjini Nairobi, Kenya, kwenye eneo la maduka katika mtaa wa Westlands.
Walioshuhudia tukio hilo, wanasema kuwa maguruneti piya yalitumika.Inaarifiwa watu watano wamekufa.
Mwandishi wetu mjini Nairobi anaeleza kuwa washambuliaji inaarifiwa walivaa vilemba kama vya al-Shabaab, lakini haikuthibitishwa kama wapiganaji hao wamehusika.
Polisi waliojihami kwa silaha wamezingira jengo la maduka liitwalo Westgate, katika mtaa wa Westlands, na kuna taarifa ya watu waliojeruhiwa wakitolewa hapo kwa machera.
Inaarifiwa kuwa watu wengi wamenasa ndani ya jengo.
Magari yaliyoegeshwa nje ya maduka yameharibika.
|
0 Comments