Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) Dk. Aloyce Nzuki (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya African Future Forum (AFF) Heunsu Kim (wa pili kushoto) wakitia saini makubaliano ya kuisaidia Tanzania kujitangaza kiutalii katika nchi ya Korea ya Kusini na kufungua ofisi ya utangazaji kwa ajili ya utalii katika mji wa Seoul. Wanaoshuhudia zoezi hilo ni wafanyakazi kutoka ofisi ya TTB na AFF, wakwanza kulia waliokaa ni George Kizeba ambaye ni Mkurugenzi wa AFF upande wa Tanzania na wa nne ni Chris Chae ambaye ni Katibu Mkuu wa AFF Afrika.
Katibu Mkuu wa Taasisi ya African Future Forum (AFF) upande wa Afrika Chris Chae (kushoto) akimuelekeza kitu Mkurugenzi Mtendaji wa AFF Heunsu Kim (kulia) ili aweze kutia saini makubaliano baina yao na Bodi ya Utalii nchini (TTB) ya kuisaidia Tanzania kujitangaza kiutalii katika nchi ya Korea ya Kusini na kufungua ofisi ya utangazaji kwa ajili ya utalii katika mji wa Seoul. Utiaji saini huo ulifanyika leo katika hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii nchini (TTB) Dk. Aloyce Nzuki (kulia) akibadilishana na Heunsu Kim ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya African Future Forum (AFF) nakala za makubaliano ya kuisaidia Tanzania kujitangaza kiutalii katika nchi ya Korea ya Kusini na kufungua ofisi ya utangazaji kwa ajili ya utalii katika mji wa Seoul. Utiaji saini huo ulifanyika leo katika hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.Picha na Anna Nkinda - Maelezo.
0 Comments