Rais Kenyatta anakabiliwa na kesi inayoanza kusikilizwa mwezi Novemba
Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika uliofanyika Ehiopia
umetaka mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai (ICC) huko The Hague
icheleweshe kesi ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, iliyopangwa kuanza kusikilizwa
Novemba mwaka huu.
AU pia wamekubaliana azimio linaloeleza kuwa hakuna kiongozi mkuu wa taifa la
Afrika aliyeko madarakani atakayefikishwa katika mahakama hiyo.
Wakati viongozi wa Kenya na Sudan wakikabiliwa na kesi huko ICC, viongozi wa
nchi za Afrika wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu kuwa mahakama hiyo inafanya
upendeleo na kuwaonea kwa makusudi.
AU ilijadili uwezekano wa nchi wanachama kujitoa, lakini wazo hilo
halikuungwa mkono kiasi cha kutosha.
Wanasiasa na wanadiplomasia waandamizi akiwemo aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja
wa Mataifa, Kofi Annan wamekosoa mpango wa kujitoa kutoka ICC.
Kucheleweshwa
Viongozi hao wa AU, waliokutana Addis Ababa, walikubaliana kuwawekea kinga ya
kutoshitakiwa kiongozi yoyote wa taifa la Afrika.
Pia wameitaka Kenya iandike barua kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataiga
kuomba ucheleweshwaji wa kesi katika mahakama ya ICC dhidi ya Rais Uhuru
Kenyatta, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya jinai. |
0 Comments