Shukrani kwa waTanzania wote  na Jamii kwa ujumla kwa kuonyesha upendo wao mkubwa wa kufanikisha Michango kwenye msiba wa ghafla uliomkuta kaka yetu, ndugu yetu, jamaa yetu, Bwana Alex Kassuwi aliyefiwa na mkewe MARTHA SHANI, siku ya Jumamosi Oct 19, 2013 kwenye hospitali ya huko Frederick Maryland.

Watanzania waishio DMV wakiushindikiza Mwili wa marehemu Martha Shani ndani ya kanisa la Good Samaritan Lutheran Church lililopo Greenbelt Maryland kwa ajili ya maombi

Kwa wale waliokua wanafuatila vyema msiba uliomkumba mTanzania mwenzetu Bwna Alex Kassuwi. Mwili wa marehemu utasafirishwa kesho kuelkea Tanzania.

M/Mungu amjalie makaazi meema Peponi Ameen


Anko George Sebo akisoma ratiba ya ibada ya Marehemu Martha Shani katika Kanisa la Greenbelt Maryland nchini Marekani


Balozi  wa Tanzania nchini Marekani Mh. Liberata Mulamula akiwa na ofisa wa balozi Mhe. Suleiman Saleh.


Mchungaji Nicodemus  Hanje akitoa neno la faraja

Mfiwa Alex Kassuwi akiwa na wanawe Joseph Kassuwi mwenye miaka 13 na Christian Kassuwi miaka 3 wakisikiliza neno la Mungu.