Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa somo kwa vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini kuhusu namna wanavyoweza kutumia fursa zilizopo kupambana na umasikini na tatizo la ajira wakati wa mdahalo wa Wiki ya Vijana leo mkoani Iringa.
 Mbunge wa jimbo la Mchinga Mh. Saidi Mtanda akizungumza na Vijana wakati wa mdahalo leo mkoani Iringa.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi akizungumza waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa leo kuhusu Wiki ya Vijana, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere na sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2013 zitakazofanyika katika uwanja wa Samora mjini Iringa .
Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.