Juu na chini ni Waziri wa fedha na Uchumi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. William Mgimwa akilakiwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Liberata Mulamula mara tu alipowasili leo Jumamosi Oct 5, 2013 kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia. Mhe. Mgimwa anaongoza ujumbe wa Tanzania kuhudhuria mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia inayoanza Jumatatu Oct 7 hadi 12, 2013 Washington, DC