Marehemu Albert Mangweha 'Ngwair'.
Arobaini ya Mwanamuziki Albert Mangweha 'Ngwair' aliyefariki Mei 28, 2013 nchini Afrika Kusini, inafanyika leo nyumbani kwao Kihonda mkoani Morogoro. Arobaini hiyo inafanyika leo ikiwa ni takribani miezi sita tangu kifo chake kwa utaratibu wa kabila la Wangoni ambao hufanya arobaini za ndugu na jamaa katika ukoo kwa utaratibu maalumu na leo ndiyo zamu ya Ngwair!