Mtaalamu wa michezo ya Karate na Yoga mtanzania Sensei  Rumadha Fundi siku ya jumamosi  November 16, 2013 
Alitoa semina maalum ya mafunzo kuimarisha viungo kutumia vifaa  asilia toka Okinawa  "Chishi na jar" kuimarisha miguu, vidole na misuri yamapaja na miguu. Mafunzo haya yana lengo la kuimarisha nguvu za mateke na utumiaji wa ngumi, na kujenga msingi wa "Kata" bora. Okinawa Goju Ryu Karate- Do "Special training for weight and conditioning" Sugarland, Texas, USA.
Sensei Rumadha Fundi (Black belt,3dan) ni mtaalamu wa mda mrefu katika michezo ya Karate ambaye alipata mafunzo
ya mwanzo katika Dojo la Zanaki,jijini Dar-es-salam nchini ya mwalimu wake Marehem Sensei Nantambu Kamara Bomani.
baadaye mafunzo ya Yoga nchini,Mafunzo ya juu na falsafa ya Goju Ryu kule Okinawa,Japan na kutunikiwa dan tatu.
Sensei Rumadha Fundi ni mmoja wa wataalamu wa kiafrika wachache wanaokubalika kimataifa katika fani hii Karate,
Pia ameweza kuendesha mafunzo na semina katika nchi mbali mbali duniani.
SENSEI RUMADHA FUNDI KUTOKA USWAHILI NI MTALAAMU WA KUJIVUNIA KWA WATANZANIA
unaweza kujiunga nae at www.facebook.com/fundi.romi

Bi.Anita Mke wa Sensei Rumadha akimpa Pongezi Mumewe katikati kwa kumaliza kazi.