Picha hii inanipa hisia tofauti na kujiuliza maswali mengi kichwani,ila majibu ya maswali hayo ninayojiuliza majibu tutayapata hapa chini,twende pamoja msomaji wangu.
Wiki iliyopita tuliishia hapa kwenye haya maandishi ya Bluu

Viongozi wachache kwenye nchi masikini huwa wanakumbuka walikotoka na hujitahidi sana kupigania haki za wanyonge na watu wenye ari duni kimaisha ila kuna wengi huwakatisha tamaa wachache wenye machungu na wenzao kwa kuwapaka mafuta na harufu nzuri ya kuwapumbaza ili wajiunge nao kuwasahau wanyonge.
Tunaendelea

UMUHIMU WA ELIMU KWA NCHI MASIKINI {sehemu ya 2}
Sio kweli kwamba elimu uliyonayo wewe ikasababisha kuwadharau wenzako kwa kipato chako au thamani zako unazomiliki,sikubali kwamba kupata kwako madaraka itakusababisha kusahau dhiki na matatizo uliyopitia kipindi cha nyuma.

Jaribu kuwaelimisha wenzako kupitia njia tofauti ili mradi nao wajikwamue kwa namna moja au nyingine,sio kwamba wote mtakaa ofisini kutokana na elimu mliyonayo,hata mfanyabiashara akipata elimu nzuri ataweza kuiendesha biashara yake vyema.Hata yule muuza magazeti,maandazi,mihogo na wamachinga wakipata elimu nzuri wataweza kuyaendesha maisha yao vizuri na kupata mbinu za kuzikuza biashara zao tofauti na kwamba wakiwa hawana elimu na matokeo yake wanajiona wanyonge na kudai kila siku wanaonewa,wanashindwa kudai haki zao vyema kutokana na kuonekana watu wa chini na hawana elimu.

Elimu ni nuru,Elimu ni ufumbuzi,elimu ni ujanja na elimu ndio kila kitu kwa kukuongoza wewe vyema katika dunia yetu ya sasa,Nchi nyingi duniani hivi sasa zinajiendesha vyema kutokana na elimu wanayokuwa nayo,nchi nyingi zinajivuna hivi sasa kwa kuwa juu kutokana na kuwa na watu wasomi,kila kukicha vitu vipya vya kisasa ambayo  madukani vinashangaza watu wengi,tofauti na siku za nyuma ni nchi chache ambazo zilionekana kuwa na wasomi na maendeleo yalikuwa ni yao kwa wao tu.

Hivi sasa kila kona ya dunia wengi wa wasomi wanapatikana ila katika bara la Africa ambalo sijui ni lini litajikwamua kutokana na sifa dhaifu ya umasikini.Zamani watu hawakupewa uhuru wa kujua mengi na kuminywa pale wanapojaribu kuyafumbua macho yao ili waone dunia inasemaje,watu hawakuwa na uhuru hata wa kuongea kwani mtu akionekana anauchongoa mdomo wake basi mwisho wake alikuwa anaujua yeye na malaika wake.

Vijana wengi siku za hivi karibuni wamekuwa wakijihusisha sana na utumiaji wa madawa ya kulevya,hii inasababishwa na kutopata elimu ya kutosha hivyo ni rahisi kushawishika kufanya mambo ambayo hayakuwa matarajio yao,sio wote kwamba walipenda kutumia madawa ya kulevya ila wengi wao kutokana na udhaifu wa akili zao wamejikuta wakiingia kirahisi katika uvutaji wa madawa hayo.

Wasichana wengi hivi sasa kila mmoja ana tamaa ya kuwa maarufu na kutajirika kirahisirahisi hali yakuwa hana hata elimu ya kutosha kwa mambo anayoyataka,sio rahisi kuwa tajiri kwa njia za mkato,hata hao matajiri wa zamani kidogo wanakupa historia zao jinsi walivyosota mpaka kufikia hapo haikuwa kazi rahisi.Unaweza kuwa maarufu kwa njia tofautitofauti inategemea una fani gani katika jamii ila kumbuka hakuna njia ya mkato katika safari ya maisha.watu wachache kwa miaka ya hivi sasa kuwa na utajiri kwa njia hii tunazoziita njia za panya.

Nawasihi sana viongozi wa Africa kuwasaidia sana wananchi wao kwa kuwapa elimu ya kutosha ili kufanikiwa kwa rahisi kimaisha na kuendesha nchi vyema.Migogoro mingi barani Africa inatokana na wengi wao kutopata elimu,watu hawajiulizi kwanini bara kama la ulaya hawapigani hovyo?,kwanini America hawapigani? na kwanini sisi waafrika tunapigana? Umasikini uliotapakaa barani Africa hakuna hata nchi moja yenye kuweza kutengeneza silaha za kivita ila kwa kwenye mapigano utashangaa zinatoka wapi na zimeingiaje ili kuja kutupiganisha wenyewe kwa wenyewe..Elimu ni jambo la muhimu katika nchi masikini barani Afrika.

         Leo tutaishia hapa mpaka juma lijalo.
         Makala hii imeandikwa na Maganga One.
                Magangaone@gmail.com