Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Gregory Teu  (kushoto) akiwasili katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mapema hii leo, kulia ni mbunge wa Rombo (CHADEMA) Mh. Joseph Selasini. 
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Godluck Ole Medeye akiwasili katika viwanja vya bunge mapema hii leo kuhudhuria  mkutano  wa kumi na tatu wa bunge unaoendelea mjini Dodoma.Picha zote na Eliphace Marwa ,Maelezo Dodoma
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiteta jambo na Mh.Sadifa Juma mbunge wa Donge mapema hii leo bungeni mjini Dodoma.


========   ========   =========

Frank Mvungi-Maelezo Dodoma

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendeelea kutoa kipaumbele kwenye Sekta ya Uvuvi ili kuwawezesha wavuvi wadogo kupata zana za kisasa. Hayo yamesemwa na Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mh.Dr. Mathayo David Mathayo wakati akijibu swali la mbunge wa (CUF) viti maalum Mh.Amina Abdallah aliyetaka kujua kwa nini Serikali Haiwezeshi wavuvi wadogo zana za kisasa .

Akitoa ufafanuzi wa hatua zilizochukuliwa Dk Mathayo alisema wavuvi wadogo 4,000 waliwezeshwa kutekeleza miradi ya uvuvi 240 na Serikali imeshaainisha maeneo ya utekelezaji unaolenga kuwa na uvuvi wenye tija ambayo ni pamoja na mradi wa usimamizi wa mazingira ya bahari na ukanada wa pwani (MACEMP).

Aliongeza kuwa zaidi ya shilingi milioni 300 zimewanufaisha  wavuvi 634 wanaoishi katika bahari za mafia, Ghuba ya mnazi na maingilio ya mto Ruvuma waliopewa ruzuku ya kununua injini za boti 22,madema 20,maboya26,000,boti 28 za uvuvi na nyavu 1,403 .

Dr. Mathayo alibainisha kuwa Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ilitoa zaidi ya milioni 59 kwa vikundi 8 kwa ajili kununulia injini za boti  na  zana za uvuvi . Akifafanua zaidi Dr. Mathayo amesema  katika eneo la mbambabay kutajengwa kiwanda cha kutengeneza boti ili kuwawezesha wavuvi wadogo kupata boti imara na zana bora za uvuvi.


Katika kuendeleza Sekta ya Uvuvi Dr. Mathayo  anasema kwa mwaka wa fedha 2013/14 Serikali itaanzisha mfumo wa kutoa ruzuku kwa wavuvi wadogo wadogo ili waliosajiliwa ili kuwawezesha kununua zana bora ambapo chini ya utaratibu huu maboti 50 na viambata vyake na nyavu za uvuvi 15,562 vitatolewa kwa wavuvi.