MWAKA 1992 alipokuwa akikabiliwa na mashitaka ya kumbaka mrembo Desiree Washington aliyekuwa na umri wa miaka 18 na aliyekuwa mshiriki katika kinyang’anyiro cha Mrembo wa Marekani, bondia mkongwe, Mike Tyson, ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 25, alijikuta akikimbilia kwa waganga wamwokoe asipatwe na kifungo cha miaka 60 jela.Hayo ameyaandika Tyson katika kitabu cha simulizi ya maisha yake kiitwacho  ‘Mike Tyson: Undisputed Truth’ kilichochapishwa leo ambapo anasema alizunguka sehemu mbalimbali akitafuta waganga wa kumwokoa na adhabu hiyo.
Katika tukio moja alikwenda kwa ‘sangoma’ wa kike ambao alimwambia ili kuokoka kifungo alilazimika kuweka noti tano za dola mia moja kila moja katika chupa halafu azikojolee na kuiweka chupa hiyo chini ya kitanda chake kwa siku tatu.
Pia alikwenda kwa mganga ambaye alikuwa ni padri  lakini akagundua alikuwa mwongo.  Alikwenda kwa waganga wengine ambapo aliambiwa kutoka usiku akiwa na njiwa na yai ambavyo alivitupa ardhini na kumwachia njiwa  na yeye kupiga kelele akisema: “Tuko huru!”
Hata hivyo, aliishia kufungwa miaka sita ambapo alitumikia miaka mitatu.
Pamoja na kufungwa, Tyson anasema adhabu hiyo iliyaokoa maisha yake kwani alipotoka alikuwa hana tamaa za kijinga za  kufanya ngono, isitoshe muda mfupi baadaye baada ya kutoka jela alijiingizia mamilioni ya fedha yaliyowafanya mastaa wengi wa kike kumfuata wenyewe.
Katika kitabu hicho, Tyson anaelezea maisha yake yaliyokuwa yamejaa uhalifu na kila mara kukamatwa na polisi.
                                                                                 Chanzo: KTN