Picha hii inanipa hisia tofautitofauti,sijui yupi mwenye akili,yupi hana,yupi katoka katika famili nzuri na yupo katoka familia duni,nani atakuwa kiongozi na nani atakuwa mnyonge.NANI MSICHANA NA NANI MVULANA!!!wangapi wasichana na wangapi wavulana,ni wote wasichana? au wote ni wavulana? Endelea kuwa nami ndugu msomaji..
Katika ari ya ya kawaida binadamu lazima upitie hatua muhimu za ukuaji kimwili na kiakili,Suala la ukuaji kimwili uanzia nyumbani ambako unapata malezi ya wazazi au walezi.Tukija katika ukuaji wa kiakili tunapaswa kushiriki kujifunza masomo tofauti shuleni ili kupata uwezo bora na mzuri katika kufikiri.Ili akili ifanye kazi sawasawa inakupasa kufundishwa masomo mchanganyiko ili kujijua au watu wakujue  uwezo wako wa akili.

Kuna baadhi ya watu hujaaliwa kipaji cha kujua uwezo wao wa akili,ila kadhalika kuna wengi wa watu wana mapungufu katika kujijua uwezo wao wa akili una ukomo kiasi gani..Sio tatizo kubwa kwa wale wenye uelewa kwamba wana mapungufu katika suala zima la ukamilifu wa akili zao,kwani watu wa aina hiyo ni vyepesi kuwasaidia na kuwaweka vizuri ili kuwa na uwezo mzuri katika suala zima la akili.Kuna baadhi ya watu wana kipaji kikubwa sana katika uwezo wa kufikiri na hao tunawaita watu wenye akili,kuna baadhi ya watu huwa tegemezi katika jamii kadhalika nao hutegemewa katika baadhi ya mambo.

Elimu.
Leo napenda nizungumzie suala la elimu kwa nchi ambazo hazina uwezo [nchi masikini]. Viongozi wengi katika nchi masikini duniani wametoka katika ari duni,msoto wa maisha wanaujua ndani nje.. yani hakuna haja ya kuwasimulia na cha kushangaza ni pale wanapopata bahati ya kuukwaa uongozi halafu wanajisahau kwa kiasi kikubwa mpaka kuwafanya wananchi wa hali ya chini kimaisha kuwafikiria tofauti.Sababu za kusema hivi zipo wazi kwani sio viongozi wachache ambao wanajisahau ni asilimia kubwa kati yao hawana uchungu tena na walala hoi kwa kile kusema wameshalewa na madaraka na utajiri walioupata kupitia udhaifu wa wenzao.

Binadaamu wa kawaida siku zote ukipitia sehemu za shida na dhiki kusahau inakuwa vigumu ila sio kwa viongozi wa nchi masikini.Kuna kitu kinaitwa mfumo wa uongozi,hiki kitu kibaya sana endapo kitaendelea kuachwa vibaya kwa viongozi kama hawa ninaowazungumzia leo hii.Hakuna sababu ya kujisahau kwamba hujui neno shida,hakuna kujisahau kwa kusema hujui nini aibu..Wengi wetu ambao tulipita kwenye shida huona huruma sana pindi ukimuona mwenzio anakulilia shida,na kama ulishawahi kupata aibu basi sina hakika kama utapenda kuona nchi yako inasifika kwa umasikini wakati wewe unawakandamiza wenzako ambao wamekupa dhamana ya kuwaongoza ili kujikwamua kimaisha.

Umasikini mkubwa wa nchi ambazo hazikuendelea unasababishwa kwa kiwango kikubwa sana na watu wa nchi hizo kukosa elimu.Binaadamu wa leo ukikosa elimu bora itakuwa ni bahati sana kufanikiwa kimaisha..Sio kwamba watu wote waliokosa elimu kwamba wamefeli maisha laa'hasha..Ila wengi wao waliopata elimu bora wana maisha bora na mazuri japo wachache hawakubahatika kufanikiwa kimaisha.Hii kwa upande wangu nasema bahati,kwani unaweza kuwa na elimu na ukakosa bahati ya kufanikiwa na ukawa huna elimu ukafanikiwa kimaisha,yote inawezekana ila kwa jitihada zako binafsi na kudra ya Mwenyezi Mungu.

Viongozi wachache kwenye nchi masikini huwa wanakumbuka walikotoka na hujitahidi sana kupigania haki za wanyonge na watu wenye ari duni kimaisha ila kuna wengi huwakatisha tamaa wachache wenye machungu na wenzao kwa kuwapaka mafuta na harufu nzuri ya kuwapumbaza ili wajiunge nao kuwasahau wanyonge.
                         Leo nitaishia hapa nawaomba niendeleze hii makala wiki ijayo.
                                      [ Makala hii imeandikwa na Maganga One Blogger ]
                                                         magangaone@gmail.com