Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na tukio la kuvamiwa na kushambuliwa Dk Sengondo Mvungi, Mjumbe wa
Tume ya Katiba. 


Waziri Nchimbi alisema upepelezi wa tukio hilo umefanikiwa kwa
zaidi ya asilimia 80 ambapo tayari watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na
mapanga na simu moja ya mkononi, watuhumiwa hao walitajwa majina yao katika
mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
jijini Dar es Salaam leo. 


Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na
waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na
uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. 


Kushoto ni Naibu Waziri
wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kulia ni Kamishna wa Polisi Kanda Maalum
Dar es Salaam, Suleiman Kova.