Kilio cha furaha kwa Moureen Julius.

Wow.....!!!...Hongera Mwanangu.

 Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi. Fatema Jaffer, akikabidhi kitita cha Shilingi Milioni tano za Kitanzania kwa Supa Staa wa Shindano la "MO Kids Got Talent 2013" Moureen Julius (12). Wanaoshuhudia tukio hilo ni baba mzazi wa Moureen pamoja naAfisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko ambao ndio waandaji wa shindano hilo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko, akiwa ameongozana na Supa Staa wa Shindano la "MO Kids Got Talent 2013" Moureen Julius (12) huku nyuma yao wakiwa na ulinzi mkali kuelekea kuzungumza na waandishi wa habari.