Mjukuu wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, Nandi Mandela, Picha AFP
Qunu.
Mjukuu wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, Nandi Mandela ameungana na waombolezaji wengine, akieleza kwamba babu yake atakumbukwa kama alama na kielelezo cha kujali utu na uwajibikaji.
Akizungumza na Shirika la Habari la AFP wakati wa maziko ya Mandela kijijini Qunu, Estern Cape jana Nandi alisema: “Tatamkhulu” inamaanisha Babu na kama ilivyo kwa Waafrika Kusini na watu wa ulimwengu mzima, tunajivunia mafanikio yake na ametufanya tujione kwamba ni watu wa pekee wa kumfanya yeye pia ajivunie uwepo wetu.”
“Mandela alionyesha ujasiri wa kipekee katika kusisitiza umuhimu wa kuheshimu tu pale kiongozi wa chama cha Kikomunisti cha Afrika kusini, Chriss Hani alipouawa Aprili 1993 na kuiweka nchi katika hatari ya vurugu na mauaji, alipoamuru watu wawe watulivu na kutii agizo lake,” alisema.
Chriss Hani alikuwa ndiye Kamanda Mkuu wa Jeshi la Umkotho we Sizwe lililoanzishwa na Mandela na baadaye alikuwa kiongozi wa chama hicho cha kikomunisti.
Binti huyo ambaye alikuwa karibu sana na babu yake wakati wa uhai wake, alieleza kwamba hata baada ya aliyekuwa Rais wa Chama cha Rugby, Louis Luyt kumpeleka mahakamani kwa hila aliwataka watu kuwa watulivu na walitii.
Alisema Mandela alikuwa kiongozi wa kweli aliyewatumikia watu kwa moyo na kwa nia ya kuboresha maisha ya walionyimwa fursa na aliwapenda watoto wake na wajukuu pia.
|
0 Comments