“PRESS RELEASE” TAREHE 26.12. 2013.
WILAYA YA MBARALI – AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA BAISKELI NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 25.12.2013 MAJIRA YA SAA 13:45HRS HUKO MBALIZI, KATA YA BONDE LA SONGWE, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA, GARI NO. T.692 BSQ/T.592 BRC AINA YA SCANIA LIKIENDESHWA NA ISMAIL S/O MOHAMED, MIAKA 42, MYAO, MKAZI WA MBAGALA LILIMGONGA MPANDA BAISKELI {MTOTO} AITWAYE KESTO S/O MAGAWALA, MIAKA 9, MSAFWA NA MKAZI WA MBALIZI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA IFISI. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI HASA KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI. AIDHA ANATOA WITO KWA MADEREVA KUEPUKA MWENDO KASI KWANI UNAUA NA KUSABABISHA MADHARA MAKUBWA.
WILAYA YA KYELA – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 25.12.2013 MAJIRA YA SAA 06:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA NKUYU, KATA YA BUJONDE, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA SADOCK S/O LIVINGSTON, MIAKA 22, KYUSA, MKULIMA NA MKAZI WA NKUYU AKIWA NA BHANGI KILO 02 NA KETE 09 SAWA NA UZITO WA GRAM 45. MTUHUMIWA ALIIFICHA BHANGI HIYO KATIKA MFUKO WA SANDARUSI. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI HIYO. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII HASA VIJANA KUACHA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA WAKULIMA KUACHA KULIMA BHANGI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJIKITE KATIKA UKULIMA WA MAZAO YA CHAKULA NA BIASHARA.
Signed by:
[B.N.MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.