Matokeo hayo yanaonyesha kuwa kati ya wanafunzi hao waliofanya mtihani huo, wanafunzi 130 wamefaulu kwa kupata alama A kwa masomo yote matano.
Mkoa wa Dar es Salaam umekuwa wa kwanza kitaifa katika matokeo ya darasa la saba huku wanafunzi wote kumi bora kwa wavulana na wasichana wakitoka katika Shule ya Tusiime ya jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotangazwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam juzi, Theresia Mmbando, mkoa huo, umevuka lengo la asilimia 60 katika mwaka 2013.
Taarifa hiyo iliwataja wanafunzi kumi bora katika kundi la wavulana kuwa ni Hussein Hemed, aliyepata alama 243, Andy Kabelege (242), Ashrak Mbondela (242), Kelvin Maseke (242), Sylivester Masimbani (242), Alex Mkwizu (241 na Basil Rweyemamu (241).
Wengine ni Jabir Jabir (241), Issa Salum (240), Franco Choma (239), Jeremiah Mkhomoi (239), Kennedy Assenga 239 na Thobias Chagula (239).
Wasichana kumi bora ni, Alice Zayumba (240), Jemmy Ndunguru (240), Maria Njau (240), Kija Ngalula (239), Fakhta Abdallah (238), Gift Mbwilo (238), Janeth Mushongi (238), Lilian Katabaro (238), Neema Miraji (238), Ahurila Kahatano (237), Aisha Daudi (237), Amina Khalfan (237), Khadija Hoza (237), Lilian Kamanzi (237) na Nyanzobe Makwaia (237).
|
0 Comments