Mhe.Balozi Liberata Mulamula (kulia)akiwa katika picha ya pamoja na Mhe.Balozi Amina Salum Ali,Mwakilishi wa Umoja wa Afrika nchini Marekani (kushoto)na Mhe. Linda Thomas Green- Field,Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani anaeshughulikia masuala ya Afrika (katikati)
Mhe. Balozi Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Somduth Soborun, Balozi wa Mauritius nchini Marekani.
Mhe. Liberata Mulamula,Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(Kushoto)katika picha pamoja na Mhe.Linda Thomas- Greenfield,Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anaeshughulikia masuala ya Afrika(wa pili kushoto)na Mhe. Michael Moussa Adamo,Balozi wa Jamhuri ya Gabon nchini Marekani(wa pili kulia) na Bw.Suleiman Saleh,Afisa wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(kulia).
Rais Barack Obama amewaalika Marais 46 wa Bara la Afrika katika mkutano wa kwanza wa aina yake "US-Africa Summit" utakaowakutanisha na viongozi wa juu wa Serikali ya Marekani na kuweka mkakati endelevu baina ya Marekani na Bara la Afrika. Mkutano huo wa kihistoria utafanyika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani maarufu State Department Agosti 5-6,2014, Washington DC. Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mmoja wa katika ya viongozi kutoka barani Afrika walioalikwa katika mkutano huo.
Mkutano wa awali ulioitishwa mwishoni mwa wiki iliyopita uliongozwa na Mhe. Linda Thomas Green- Field, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika aliyeambatana na Bw. Grant Harris, Mshauri wa Rais Barack Obama katika masuala ya Afrika. Madhumuni ya mkutano huo ulikuwa ni kuwapa fursa Mabalozi wanaoziwakilisha wa Afrika wanaoziwakilisha nchi zao hapa Marekani kuchangia masuala muhimu ambayo wanaona yatakidhi kujadiliwa katika mkutano. Mabalozi kadhaa walichangia na kutoa maoni yao akiwemo Mhe. Liberata Mulamula,Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mhe.Balozi Amina Salum Ali,Mwakilishi wa Umoja wa Afrika hapa Marekani.
0 Comments