Muungano ni urithi wetu ambao tumeukuta toka kwa wazee wetu waliotangulia mbele za haki..Tuna kila sababu za kuuenzi Muungano huu na tuna kila sababu za kutufanya tufurahi kwa Muungano wetu,yale mapungufu yaliyopo tuna imani kwamba viongozi wetu watayafanyia kazi na kuziba mapengo ya mapungufu hayo.

Vijana wenzangu tusishawishike na maadui zetu wanaotuchochea kila kukicha juu ya hii tunu ambayo wao hawana,amani tuliyonayo wengi hawana na hata walionayo ni wachache kwani wengi wao wameshapoteza amani na hivi sasa wanaishi kwa mashaka tofauti na awali.

Jambo muhimu kwa vijana wenzangu ni kufahamu kwamba tunaishi kwa kanuni na sheria za nchi,haipendezi kupindisha au kudharau taratibu za nchi,tuwaheshimu viongozi wetu na kuipenda nchi yetu,tuwe na mapenzi na uzalendo wa kweli.taratibu mwishowe tutafika,hatuna haja ya haraka kwani hapa tulipo tujivunie na amani yetu,wengi wanapenda kuwa kama sisi ila ni vigumu kwani walishapoteza tunu yao ya amani kwa kushawishika na ulimwengu.

Mungu Ibariki Africa,Mungu ibariki Tanzania nzima.
Asanteni sana- Maganga One.