Moses mwanamume anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja atafuta hifadhi nchini Marekani |
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametia saini mswada wenye utata unaotoa adhabu kali kwa watakaopatikana wakishiriki mapenzi ya jinsia moja.
Rais Museveni alitia saini mswada huo nyumbani kwake katika hafla iliyoshuhudiwa na maafisa wakuu wa serikali pamoja na wandishi wa habari.Mswada huo ambao sasa utakuwa sheria, unatoa adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa wale watakaopatikana na hatia ya kuhusika na mapenzi ya jinsia moja.
Mswada huo pia umeharamisha wanaharakati kutangaza misimamo yao hadharani kuhusu au kuwasaidia wanapenzi wengine wa jisnai moja kujitangaza hadharani.
Adhabu hiyo pia itatolewa kwa wale wanaopatikana na hatia ya kuwahusisha watoto katika vitendo hivyo, walemavu au kumuambikiza mtu virusi vya Ukimwi katika mapenzi ya jinsia moja.
Mswada huo umepigiwa debe sana nchini Uganda, lakini mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yameulaani.
Uganda imepuuzilia mbali shinikio za Marekani na nchi zengine za Magharibi kutopitisha sheria kali dhidi ya vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.
Mswada huo umeweka sheria kali zaidi dhidi ya uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja kwa yeyote atakayepatikana akishiriki.
Usagaji pia umeharamishwa kwa mara ya kwanza na pia ni hatia kumsaidia mtu kushiriki mapenzi ya jinsia moja. Wanaharakati wa kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wanasema wanajiandaa kwenda mahakamani kupinga sheria hiyo mpya.
Uganda ni miongoni mwa mataifa 30 Afrika ambayo yameharamisha mapenzi ya jinsia moja. Ni wiki jana tu ambapo Rais wa Gambia Yahyah Jammeh aliyesema mapenzi ya jinsia moja ni sumu kali mno.
0 Comments