MWENYEKITI wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amefunguka kuwa anajitahidi sana kuonyesha maadili mema ili kuhakikisha wanachama wake wote wanamuiga.

Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Akistorisha na paparazi wetu juzikati, Steve alisema kuna mambo mengi ambayo alikuwa akiyafanya kabla ya kuwa rais wa klabu hiyo lakini sasa anajiepusha nayo ili kuhakikisha anajenga picha nzuri na kuwataka wanachama wamuige yeye.
“Ile dhana ya kwamba Bongo Movie kumekithiri maovu, nataka niiondoe kabisa. Ili kufanikisha hilo lazima mimi mwenyewe niwe mfano kwa kuwaonyesha wengine, nimeshabadilika na wao lazima wabadilike,” alisema Steve.