DSC_0041
Mjasiriamali na Mbunifu wa mavazi nchini Tanzania, Doreen Noni akizungumza kwenye Exclusive Interview na mtandao wa habari wa MOblog.
Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
MJASIRIAMALI na Mbunifu wa mavazi nchini Tanzania, Doreen Noni anatarajiwa kushiriki kwenye shindano la kumtafuta mbunifu bora katika sanaa ya filamu, (Africa Magic Viewers Choice Awards) nchini Nigeria wiki hii.
Akizungumza na MOblog Tanzania, hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Noni amesema kwamba amechaguliwa kushiriki katika shindano hilo la Africa Magic Viewers Choice Awards baada ya kushiriki filamu ya siri ya mtungi.
“Africa magic viewer’s choice awards ni kama Oscar ya Afrika ambapo sinema zote wanazotizama watu kwenye Mnet, series na nia hasa ni kutizama kazi za wasanii mbali katika fani ya uingizaji wa filamu Afrika,” amesema
Amesema alifanikiwa kufanya kazi na kampuni ya (Media for Development International) ambao wanafanya kazi ya kuhamasisha kazi za uzalishaji katika filamu za Afrika ili kutambua mchango wa wasanii mbalimbali katika bara hili.
DSC_0128
Noni amesema kuwa kupitia kampuni au shirika hilo lisilo kuwa la kiserikali aliweza kushiriki kwenye filamu ya “Siri ya Mtungi” ambapo alitengeneza nguo na mavazi yote yaliyotumika katika filamu hiyo.
Amesema kwamba katika filamu hiyo alitengeneza nguo kwa kila mshiriki wa filamu baada ya kuzunguka katika masoko mengi ya jijini Dar es Salaam katika kutafuta nguo zinazoendana.
“nimechaguliwa baaada ya kupeleka baadhi ya kazi zangu za kisanii hasa kwa design na kubuni mavazi mbalimbali baada ya kuonyesha kipaji chake katika tamthilia hiyo ya Siri ya Mtungi,” alilisitiza
Noni amesema kwamba yeye ana malengo yake kama kijana na mjasirimali ni kufika mbali katika fani yake hiyo ya ubunifu wa mavazi na ujasiriamali.
MJASIRIAMALI na mbunifu wa mavazi anayekuja juu nchini Tanzania, Doreen Noni anatarajiwa kushiriki kwenye shindano la kumtafuta mbunifu bora katika sanaa ya filamu, Africa Magic Choice Awards nchini Nigeria.