Naibu Waziri wa Fedha (Sera) Mhe. Mwigulu Mchemba akijibu maswali 
mbalimbali katika Bunge la Pamoja la Afrika, Karibiani na Pacific (ACP) 
na Jumuiya ya Ulaya leo jijini Strasbourg Ufaransa.   
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Mchemba (katikati) akipitia hotuba
yake kabla ya kuhutubia Bunge la Pamoja la Afrika, Karibiani na Pacific
(ACP) na Jumuiya ya Ulaya leo Strasbourg Ufaransa.  Mhe. Mchemba
anaongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao hicho na ameitaka Jumuiya ya
Ulaya kuacha kushinikiza nchi za ACP kuweka sahihi Mikataba ya Ubia wa
Biashara ambayo haina tija kwa nchi za ACP. Kulia ni Balozi wa Tanzania
Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala na kushoto ni Bi. Raymold
Dominic Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya ACP anayesimamia masuala ya
siasa.