Na Musa Mateja
Kabang! Kwa mara ya kwanza, Kikosi Kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers, kimefanikisha zoezi la kumnasa laivu Mbongo-Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, akizama na kuchukua dozi ya dawa za kuondoa sumu ya madawa ya kulevya ‘unga’ mwilini, Amani lina tukio kamili.Kazi hiyo nyingine nzuri kwa OFM ilifanyika juzi (Jumanne), majira ya saa 3:30 asubuhi ndani ya Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar ambapo staa huyo almaarufu Kiuno Bila Mfupa alifika eneo hilo kwa ajili ya kuchukua dozi hiyo ya dawa aina ya Methadone.OFM MZIGONI
Awali, miezi miwili iliyopita, Amani lilidokezwa kuwa Ray C amekuwa akionekana hospitalini hapo hivyo kachero wa OFM kutakiwa kuthibitisha juu ya habari hiyo.

Kachero huyo alianza kumfuatilia staa huyo wa Wimbo wa Na Wewe Milele  hatua kwa hatua lakini kila alipomvizia ilishindikana kumnasa hadi juzi, alipojaa kwenye kumi na nane.

Kilichofanyika ni kwamba kamanda huyo wa OFM aliamua kumkeshea maeneo hayo na hatimaye akambamba kilaini akizama ndani ya hospitali hiyo.RAY C LAIVU
Ray C alionekana laivu akiingia hospitalini hapo akiendesha gari aina ya Toyota Carina, majira hayo ya saa 3:30 asubuhi na akatoka saa 4:30 asubuhi ambapo muda wa kuingia na kutoka kamanda wetu alikuwa akimfuatilia kwa kuchukua picha za matukio yote hadi alipoondoka kwenye eneo la hospitali hiyo.Uchunguzi wa OFM hospitalini hapo ulibaini kwamba mwanadada huyo aliyepanga kurudi stejini muda wowote kuanzia sasa, alipofika alikwenda moja kwa moja kwenye chumba maalum cha daktari ambapo alikabidhiwa dozi hiyo ya Methadone na ushauri nasaha.
BOFYA HAPA KUMSIKIA KIUNO BILA MFUPA
OFM haikutaka kukamilisha kazi hiyo bila kusikia kauli ya mrembo huyo, hivyo ilimtafuta ili aweze kuzungumzia juu ya uchukuaji wa dozi hiyo tangu alipotangaza kuachana na madawa ya kulevya kwa msaada wa Rais wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
Alifunguka: “Ni kweli nina kawaida ya kwenda kuchukua dawa kila siku asubuhi kwenye Hospitali ya Mwananyamala, Dar maana ndicho kituo nilichopangiwa tangu nilipoachana na utumiaji wa madawa za kulevya.
“Kwa sasa hali yangu iko safi yaani naweza kusema nimeshapona moja kwa moja isipokuwa nakamilisha dozi yangu tu.
“Pia nipo kwenye mpango wa kuanza kuzunguka karibu Tanzania nzima ili niweze kutoa elimu kwa waathirika wengine wa madawa ya kulevya.
“Kuhusu mpango huo, tayari nimeshafungua ofisi kwa ajili ya kusimamia Foundation (taasisi) hiyo na nimetoa fursa kwa Watanzania waweze kunitumia nembo au logo nzuri na atakayeshinda mwisho wa mwezi huu atapata shilingi laki tano kama zawadi.
“Nafarijika sana na watu wote walionipigania hadi leo ninajitambua kama hivi, ingawa kuna watu wengi sana walikuwa hawaamini juu yangu kama kweli ningeweza kuachana na utumiaji wa dawa za kulevya hadi kufikia kiasi hiki, hivyo basi mizunguko yangu ya kuelimisha watu hawa itakuwa kama moja ya fadhila yangu kwa Mungu na wote walionipigania kwa hili.”
MADAI YA KURUDIA UNGA
“Hilo siyo kweli kwa sababu kwanza nitaharibu dozi na pia madaktari wangejua. Siwezi kurudia kwani najua mateso niliyokutana nayo na pia watu walivyonipigani uhai wangu,” alisema staa huyo mkubwa.
DAKTARI ANASEMAJE?
Ili kuthibisha kama amerudia au la, OFM ilizungumza na mmoja wa madaktari wanaomhudumia Kiuno Bila Mfupa kwa sharti la kutotajwa ambaye alithibitisha kuwa kwa sasa Ray C hatumii unga kwani wangemshtukia.
Popote aendapo Ray C huwa haachi kuyashukuru Magazeti ya Global Publishers kwani ndiyo yaliyoanika jinsi alivyokuwa ameathirika na unga miaka miwili iliyopita hadi akasaidiwa kwani kabla ya hapo zilikuwa ni tetesi tu kuwa anatumia ‘hiyo kitu’.