Waombolezaji wakiwa msibani Jana kushoto mwenye tisheti nyeusi ni Mratibu wa Skylight Band

William Malecela akijadili jambo na Mkurugenzi wa Skylight band Justine Ndege ili kuweka mambo sawa kabla ya Mwili wa marehemu kuwasili.

Baadhi ya waombolezaji wakibadilishana mawazo Katikati ni Mwanamuziki wa Skylight band Joniko Flower.

Waombolezaji wakiendelea kubadilishana mawazo wakati wakisubili mwili wa marehemu Kufika,Mwenye Baibui nyeusi ni mke wa Chicago Matelephone na wanamuziki wa Skylight band

Mkurugenzi wa Skylight Band akijadili jambo na Aneth Kushaba ili kuweka mambo sawa kabla ya Mwili wa marehemu kuwasili.

Gari iliyobeba Mwili wa marehemu Chiri Challa likiwasili Nyumbani kwa marehemu


Ndugu na Jamaa wakishusha Mwili wa marehemu Chiri Challa

Mwili wa Marehemu ukishushwa kwa ajili ya ibada

Mchungaji wa kanisa alipokuwa Anasali marehemu akiongoza ibada ya kumuombea Marehemu Ayoub Songoro maaru Chill challa aliyekuwa mwanamuziki na mpiga Gita wa Skylight Band.

Misa ya kumuombea Marehemu ikiendelea Nyumbani kwake Mwananyamala

Mke wa marehemu akiwa na majonzi

Meneja wa bendi Ya Skylight Aneth Kushaba akiaga mwili wa marehemu

Waombolezaji wakiaga mwili wa marehemu

Mkurugenzi wa Skylight Band Justine Ndege akiaga Mwili wa marehemu

Watoto wa marehemu wakiwa na majonzi ya kuondokewa na baba yao kipenzi

Kaka wa marehemu akiaga mwili wa mdogo wake kwa huzuni kubwa

Mwili wa marehemu ukipandishwa kwenye gari Tayari kwenda kuzikwa baada ya ibada ya kumuombea

Msafara ukielekea makaburi ya Mwananyamala kwa kopa

Mwili wa marehemu ukishushwa kaburini tayari kwa kuzikwa

Wanamuziki wenzake na marehemu wakifuatilia mazishi ya mwenzao

Mchungaji akisoma neno

Mchungaji akirusha udongo kuonyesha ishara ya kuaza maziko

Mke wa marehemu akirusha udongo ndani ya kaburini

Watoto wa kiume wa marehemu wakirusha udongo kaburini kumzika baba yao

Kaka wa marehemu akiwa akimzika mdogo wake

Mkurugenzi wa Skylight Band Justine Ndege akirusha udongo kumzika msanii wake

Meneha wa Skylight Band Aneth Kushaba akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu

Waombolezaji wakiwa wanafuatilia maziko kwa huzuni kubwa

Mchungaji akiweka msalaba kwenye kaburi la marehemu.
Untitled

Mke wa marehemu akiweka shada la maua kwenye kaburi

Watoto wa marehemu wakiweka shada la maua kwenye kaburi na Baba yao

Ndugu wa Marehemu wakiweka Shada la maua.

Mpiga Gitaa mahiri wa bendi ya Skylight Chiri Challa amezikwa Ijumaa kwenye makaburi ya Mwananyamala kwa Kopa na mamia ya watu na wanamuziki wenzie.Marehemu Chiri Challa alifariki Tar 17-04-2014 hospitali ya Taifa ya Muhimbili.Chanzo cha kifo cha marehemu ni shinikizo la damu ambapo kabla ya kifo chake alikuwa katika afya njema, lakini Usiku wa Tar 16 marehemu alidondoka gafla bafuni na ndipo alipokimbizwa hospitalini.
Madaktari walijitaidi kwa kila hali na mali kuokoa uhai wa marehemu lakini ilishindikana kutokana na shinikzo la damu kuwa kubwa sana na ndipo Chiri challa akafariki dunia,Marehemu Chiri Challa ameacha Mke na watoto wawili, Marehemu alikuwa ni mpiga gita mzoefu na mahiri ambaye amepitia karibu bendi zote kubwa na kongwe nchini kama Akudo, Fm Academia n.k na ahadi mauti yanamfika alikuwa na Skylight Band
Uongozi mzima wa Skylight band unawashukuru wale wote waliojitoa kwenye msiba huu na Mungu awabariki.PICHA ZOTE NA DJ SEK BLOG