Watu kadhaa wameuawa wakati wa jaribio la wizi wa Ng'ombe katika jimbo la Warrap nchini Sudan Kusini.
Afisa mmoja katika eneo hilo PaulDhel Gum ameviambia vyombo vya habari kwamba takriban watu 28 wameuawa.
Amesema kuwa polisi wamewaua wavamizi wengi.
Uvamizi huo ulitekelezwa katika eneo la mashambani la jimbo la Warrap siku ya alhamisi ,na kwamba hakuna maelelzo zaidi.
Haijulikani iwapo mauaji hayo yanashirikishwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya serikali ya Sudan kusini na waasi walio watiifu kwa aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.