Kamanda Ras Makunja wa Ngoma Africa band mwanamuziki mpiganaji
aleyepachikwa majina mengi ya utani kutokana na matukio au Viumbe wa ajabu "Anunnaki Elien" yenye makao yake kule Ujerumani.
Mara nyingine Mtunzi huyu Kamanda Ras Makunja aliyeipindia akili kazi yake,anapoona nyimbo zake zimekuwa cheche za moto uwa anapooza
kwa kupeleka ujumbe mzuri kwa jamii wenye kuziteka nyoyo za wengi
na kuweza kuzipiga masaji roho za walio wengi "Bongo Tambarare"
hapo kamanda Ras Makunja na kikosi chake Ngoma Africa Band wanaonekana kuwa watoto wazuri lakini tabia zao ni kama ngozi hazibadiriki wawapo jukwaani ni sawa na askari wa kutuliza ghasia FFU, kwa sababu wanajua
wazi tabia za washabiki wao za kupenda mdundo live wenye kasi kubwa
kwa mtindo huu wamefanikiwa kuteka mamilioni ya washabiki nje na ndani ya ughaibuni.
Ras Makunja na Muzimu wake "Ngoma Africa Band" wapo ndani ya medani
ya muziki wa dansi takribani miaka 21 na kushika chati katika majukwaa
ya kimataifa.
inasemekana Ngoma Africa band ina himaya yake inayoitwa "Anunnaki Empire"
himaya ya viumbe wa ajabu (wasanii na waliowazunguka) katika makao ya bendi,wakiwemo mafundi mitambo ambao kazi yao ni kuhakikisha kila kitu
kinacho fanywa ni " Extraordinary" mpaka mziki wenyewe ni "Extraordinary Bongo Dansi" himaya yao haina uwoga bali inatishia wapinzani wao.
Mwanamuziki Ras Makunja inasemekana hatumii ulevi wa aina yoyote hile wa
kuvuta sigara au kasumba bali ni mtu wa mazoezi makali ya kimwili na kihisia,
mazoezi ambayo watu wengi wanadai kuwa yanamsaidia kuongoza kikosi chake
anaposafiri na kufanya tour ndefu,pengine katika nchi zenye utamaduni tofauti na wa afrika. Kamanda Ras Makunja kufanya nae kazi inabidi uwe mjeshi sio mchezo,kwa sababu hana mdhaa katika kibarua chake.
hivi karibuni inasemekana amesharekodi kibao kipya kinachoitwa " Myonge Mnyongeni ! Haki yake Mpeni" wimbo ambao utatolewa baadaye.
Muziki wa bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya unasikika pia katika tuvoti at www.ngoma-africa.com piawww.reverbnation.com/
|
0 Comments