Wakuu wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakizindua kitabu rasmi cha Muongozo wa Majaji wa Jumuiya hiyo kwenye Mkutano wa 12 wa siku moja wa Jumuiya hiyo uliofanyika ukumbi wa Kimataifa wa Arusha. Rais Uhuru Kenyata wa Kenya ambae ndie Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni pamoja na Mwenyeji wa Mkutano huo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Wengine ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Burundi Bwana Bazombasa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyemuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohd Sheni pamoja na Waziri Mkuu wa Rwanda Bwana Pierre Damieni Habumuryemi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa niaba yaRais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Sheni akipokea kitabu wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mkoani Arusha.

Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania waliohudhuria Mkutano wa 12 wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki huko Arusha. Wa mwanzo kutoka kushoto ni Waziri wa Ardhi wa SMZ Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Mh. Benard Membe na Waziri wa Afrika Mashariki Mh. Joh Samuel Sitta.
 Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA