Katika kuonyesha hali ya kuwajali watu wa nyumbani Tanzania walio katika mazingira magumu ya kiafya na mambo muhimu ya mahitaji ya binaadamu,kikundi cha Upendo Womens Group kilichopo jijini Brussels nchini Belgium kimeandaa chakula cha jioni kitakachokutanisha mataifa mbalimbali wakiwemo watanzania wenyewe.


Lengo ni kuchangishana kwa kile tulichoaajaliwa ili kuwasaidia ndugu zetu wanaopata shida katika mambo muhimu ya msingi katika jamii..

Balozi Kamala atakuwepo.
Balozi wa Tanzania nchini Belgium Mh:Kamala ni mmoja wa wageni waalikwa siku hiyo,kwa hivyo ni fursa yako ndugu mtanzania kukutana na Balozi wako kwenye tafrija hiyo.

Ngoma za Asilia na Taarabu
Kutakuwa na ngoma za kiasili na Taarabu kwa siku hiyo hapo ukumbini.

Chakula 
Kutakuwa na Buffet na kila mmoja aamini kwamba atafurahia chakula siku hiyo.

Muziki
Patachezwa muziki kwa kila mwenye kupenda muziki

Muda
Shughuli zitaanza saa kumi kamili jioni16:00 na kuisha saa tano za usiku 23:00.
Itapendeza kama ukija na wenzako wengi ili kuonyesha upendo kwa wanaupendo wa umoja huo.

Ukiliona tangazo hili hautapata dhambi ukimwambia na mwenzako.
Watu wote mnakaribishwa.