Mtoto Neema Joseph alivyokuwa kabla ya kufanyiwa upasuaji
Neema ambaye anaishi na mama yake Anastazia Yohana (28) katika Kijiji cha Bugomba, Kata ya Bulungwa wilayani Kahama, Shinyanga, kabla ya kupata tiba, alikuwa akilia kwa maumivu kufuatia jicho hilo la kulia kuvimba na kutoa usaha kila siku hali iliyomtesa mzazi huyo pia.
Baada ya kuhangaika katika hospitali tofauti bila kupata tiba sahihi, mama wa Neema ambaye alifiwa na mumewe na kukosa msaada wowote kutoka kwa ndugu wa mwanaume, alishauriwa kumpeleka mtoto huyo katika Hospitali ya Bugando, Mwanza kwa matibabu.
Kwa kuwa hakuwa na uwezo, Aprili Mosi, mwaka huu, shukurani ziende kwa gazeti mama la hili, Uwazi ambalo lilikuwa la kwanza kuchapisha habari ya mtoto huyo hivyo wasamaria wema walioguswa na mateso ya Neema walimchangia fedha za matibabu kupitia Shirika la Huheso Foundation la mjini Kahama.Katika michango hiyo, zilipatikana shilingi 1,500,000 (milioni moja la laki tano) ambazo zilimwezesha kupelekwa kwenye Hospitali ya Bugando ambako alilazwa na kuanzishiwa dozi ya sindano huku akisubiri kufanyiwa upasuaji.
Mama Neema alisema anamshukuru Mungu kwani tangu alipofika hospitalini hapo, alipopimwa alipata tiba ya dawa ambazo zililiponya jicho hilo lililokuwa limevimba kwa nje na kurudi ndani katika muonekano wake wa kawaida.
“Nashukuru Mungu kwani alikuwa akilia sana kutokana na maumivu makali ambayo alikuwa akiyapata kila siku.“Ilikuwa hatulali maana unamuona kabisa mtoto anateseka na wewe huna namna ya kufanya, jicho lilikuwa likitoa harufu kali lakini kwa sasa namshukuru Mungu anaendelea vizuri,” alisema mama Neema.
Mama Neema aliishukuru Kampuni ya Global Publishers Ltd wachapishaji wa magazeti ya IjumaaWikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi kwa kuchapisha habari hiyo ambayo iliwagusa watu na kumchangia.
Baada ya tiba hiyo ya awali ya sindano, mtoto Neema anatarajiwa kufanyiwa upasuaji ili kuangalia uwezekano wa kumaliza kabisa tatizo alilonalo.
|
0 Comments