Na Mwandishi Maalum, New York
Wakati wajumbe wanaoshiriki mkutano wa tathmini kuhusu Mkakati wa Umoja wa Mataifa dhidi ya ugaidi wakilaani matukio ya kigaidi yanayotekea katika nchi mbalimbali, baadhi ya wajumbe hao wametaka matukio hayo yasihusishwe na madhehebu ya dini iwayo yoyete ile.
Mkutano huo wa siku mbili umemalizika siku ya Ijumaa hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Pereira Silima ( Mb).
Wakati wote wa majadiliano kuhusu mkakati huo uliopitishwa, huku kila muwakilishi wa nchi inayoshiriki mkutano huu alipopewa fursa ya kuzungumza, hakusitia kuzungumza au kulaani mwendelezo wa matukio ya kigaidi na hususani yaliyotokea hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Pereira Silima (Mb) akiwa na ujumbe wake muda mfupi kabla ya kuchangia majadiliano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu Mkakati wa kuudhibiti Ugaidi.
Mhe. Naibu Waziri Silima akilizungumza Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu mkakati wa kuukabili ugaidi, katika mchango wake Waziri alisisitiza ushirikiano wa kimataifa katika kuukabili ugaidi hasa kutokana na ukubwa wa mtandao wake. Aidha alielezea Tanzania kutoridhishwa na namna tatizo la usambaaji na matumizi holela ya silaha ndogo na nyepesi lilivyoshughulikiwa katika rasmu ya tamko la mkutano huo.
Sehemu ya wajumbe wakiwa ndani ya ukumbi wa mikutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, wakati wa majadiliano ya tathmini kuhusu Mkakati wa Umoja wa Mataifa wa Kuudhibiti Ugaidi. Mkutano huo wa siku mbili umemalizika jana Ijumaa
0 Comments