Kikosi cha Mol All Stars ambacho jana kilitoa dozi kwa Leuven

 Golikipa namba moja wa Mol All Stars  Maganga One akiokoa moja ya hatari langoni mwake hapo jana..Mol iliivuruga Leuven kwa goli 3-1.
OOooh  Kitu ndani ya net,Golikipa wa Leuven Mahsein  akikubali matokeo baada ya kushindwa kuzuia mkwaju mkali uliompita langoni kwake.
Ooooopss!! Maganga One akikubali matokeo baada ya kushindwa kuukabili mkwaju mkali uliopigwa na mshambuliaji wa timu ya Leuven hayupo pichani.
Hatari katika lango la timu ya Leuven 
Mlinzi wa timu ya Mol All Stars, Ally Q akiondosha hatari katika lango lake hapo jana,timu ya Leuven ilikubali kichapo cha goli 3-1  
Washmbuliaji hatari wa Mol All Stars wakimaliza habari kwa kufunga kurasa baada ya kutingisha nyavu kwa goli la 3.mpaka mwisho w mchezo Mol All Stars 3-1 Leuven.(picha zote na Sharon  Maganga One)

Baada ya Mechi.
Muda mfupi baada ya mchezo kumalizika,wachezaji wa kimataifa wa Mol All Stars walitoa salam kwa timu zote zinazoomba mechi zijitahidi kufanya mazoezi ya kutosha kwani zimechoka kutoa dozi kwa timu ambazo hazina upinzani wa kutosha uwajani.

Mol waliwaambia wachezaji wa Leuven kwamba hii ilikuwa zawadi tosha kwa mfungo wa Ramadhani.
Mol inategemea kuwakaribisha Oostande siku chache zijazo baada ya mfungo mtukufu wa ramadhani kwisha pindi makubaliano yakishamalizika.