Chanzo cha habari hii kutoka kwa marafiki wa Diamond kimedai kuwa Wema amenasa ujauzito na kugundulika hivyo walipokuwa Afrika Kusini kwenye tuzo za MTV-MAMA na kumfanya Diamond achanganyikiwe kwa furaha....
Kwa mujibu wa chanzo hicho, inadaiwa kuwa Diamond kwa sasa kawa kama mtu aliyepagawa kwa furaha kutokana na taarifa hizo njema na tayari ameshaanza maandalizi ya kijacho chake....
Kugundulika kwa ujauzito wa Wema ni baada ya kuanza kujisikia vibaya walipokuwa Afrika Kusini ikiwemo kichefuchefu na kizunguzungu alipokuwa hotelini alipofikia na kulazimika kwenda hospitali kwa uchunguzi zaidi....
Inasemekana kuwa Wema alisindikizwa na Aunt Ezekiel kwenda hospitalini waliyekuwa naye huko Afrika Kusini kumpa sapoti Diamond na madaktari ndiyo waliomjuza kuwa anakiumbe tumboni cha wiki 7...
0 Comments