Wanajeshi wa Iraq wakielekea mjini Tiqrit
Serikali ya Iraq inasema kuwa vikosi vyake vimeuteka mji wa kazkazini wa Tikrit kutoka kwa wapiganaji wa ki-sunni ambao walikuwa wameteka mji huo wiki mbili zilizopita.
Vyombo vya habari vya kitaifa vimesema kuwa wanajeshi wakisaidiwa na mizinga pamoja na ndege za kijeshi waliwafurusha wanamgambo wa kundi la ISIS na kuwaua zaidi ya sitini.Waasi hao wamesema kuwa kulikuwa na mapigano makali katika mji huo na kwamba mashambulizi hayo hayakufua dafu.
Iwapo itathibitishwa ,utekaji wa mji wa Tikrit utakuwa hatua kubwa ya jeshi la Iraq tangu ISIS kuyateka maeneo mengi ya Iraq kazkazini mapema mwezi huu.
Serikali sasa inasema kuwa inajiandaa kuelekea mjini Mosul ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini humo.Wakati huohuo Iraq inasema kuwa imepokea kundi la kwanza la ndege za kijeshi ilizoagiza kutoka Urusi ili kuisadia kukabiiana na wapiganaji wa dhehenu la kisunni ISIS ambao wameyateka maeneo mengi ya taifa hilo.
Wizara ya Ulinzi inasema kuwa ndege hizo 5 zenye uwezo wa kushambulia maeneo ya ardhini zitaaanza kuhudumu katika kipindi cha siku chache zijazo,huku nyingine zikitarajiwa kuwasili.