Aliyekuwa mchezaji na Kocha Msaidizi wa Manchester United, Ryan Giggs ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa Sayansi kutoka Chuo Kikuu cha Bolton, England kutokana na mchango wake mkubwa katika mchezo wa soka. Giggs kwa sasa atajulikana kama Dk.Giggs kutokana na heshima hiyo kubwa aliyoipata.